Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Marekani aondolewa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono

Muigizaji Nyota Wa Marekani Aondolewa Mashtaka Ya Unyanyasaji Wa Kingono Muigizaji nyota wa Marekani aondolewa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Muigizaji Kevin Spacey amepatikana hana hatia katika makosa yote tisa ya uhalifu wa kingono.

Muigizaji huyo aliyeshinda tuzo ya Oscar alibubujikwa na machozi wa wakati hukumu ya keshi dhidi yake ilipotolewa katika Mahakama ya Southwark Crown mjini London.

Umuzi huu umetolewa siku ambayo anasherehekea miaka 64 ya kuzaliwa.

Mara baada ya kuondolewa mashtaka Kevin Spacey amesema kuna mengi ya kuyashughulikia baada ya kile kilichotokea leo.

Anasema "anashukuru sana" jopo la mahakama kwa kuchukua muda wa kuchunguza ushahidi na ukweli wote kwa makini kabla ya kufikia uamuzi wao. "Nimeridhishwa na matokeo leo," anaongeza.

Spacey alipata umaarufu kutokana na filamu zake kama vile American Beauty na House of Cards na alikuwa mkurugenzi wa ubunifu wa ukumbi wa michezo wa Old Vic.

Muigizaji huyo aliahidi kurudi Uingereza kujitetea na kusafisha jina lake, na amefanya hivyo.

Kabla ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia kutangazwa hadharani dhidi yake mnamo 2017, Kevin Spacey alikuwa mmoja wa waigizaji waliotafutwa sana huko Hollywood.

Aliitaja kesi kuwa dhaifu, akisema watu waliomtuhumu walikuwa wakitafuta pesa kwa kutumia madai ya uwongo.

Chanzo: Bbc