Jopo la mahakama ya Los Angeles limempata mwanaume aliyekuwa na mamlaka na ushawishi zaidi katika filamu za Hollywood Harvey Weinstein na hatia ya kumbaka mwanamke.
Katika kesi hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi miwili, mahakama ilisikua ushahidi kuhusu jinsi Bw.Weinstein alivyotumia ushawishi wake kuwalaghai wanawake na kuwaingiza katika mikutano ya kibinafsi kabla ya kuwashambulia.
Weinstein mwenye umri wa miaka 70-Msindi wa tuzo ya Oscar anakabiliwa na kifungo cha miaka 24 jela atakapohukumiwa.
Tayari anatumikia kifungo cha miaka 23 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika kesi yake ya kwanza iliyomalizika mjini New York miaka miwili iliyopita.
Weinstein alipatikana na hatia Jumatatu ya ubakaji na mashitaka ya unyanyasaji wa kingono yanayomhusisha mwanamke aliyemshitaki aliyepewa jina -Jane Doe 1, ili kulinda utambulisho wake.
Jopo la mahakama halikuweza kufikia uamuzi kuhusu madai yaliyotolewa na Jennifer Siebel Newsom, mke wa gavana wa California ,Gavin Newsom, na mwanamke mwingine anayefahamika kama Jane Doe 2.
Aliondolewa mashitaka ya ngono ya lazima yaliyotolewa na mwanamke anayeitwa Jane Doe 3.