Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Hashim Kambi aula ubalozi

7b001ea99dde90295438e1fd3d1a8110 Muigizaji Hashim Kambi aula ubalozi

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MUIGIZAJI nguli wa filamu nchini Hashim Kambi, amepata nafasi ya kuwa Balozi wa kampuni ya uuzaji wa mafuta ya MUNIO ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kutumia nafasi hiyo kufanikisha malengo ya kibiashara ya kampuni hiyo.

Kambi msanii wa miaka mingi aliyejipatia umaharufu baada ya kuigiza katika filamu mbalimbali nchini, aalitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha kwanza cha kuuzia mafuta cha MUNIO kilichopo Kinyrerezi.

Alisema kama akiwa kama balozi wa kituo hicho, watahakikisha mbali na wateja wa kawaida yakiwemo makampuni wasafirishajiwa huduma za daladala, pia atawashawishi wasanii wenzake kukitumia kituo hicho kwa ajili ya kujipatia huduma borsa.

“Naushukuru uongozi kampuni hii kuniona nastahili kuwa balozi wake, imani yangu tutaendelea kushirikiana kwa kipindi kirefu kuhakikisha kila mwananchi ananufahika na huduma za uuzaji mafuta inazozitoa, hapa ni sehemu ninayoamini ina huduma zote bora kwa wananchi” alisema Kambi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho cha MUNIO Christopher Nduli alisema kufunguliwa kwa kituo hicho ni muendelezo wa mchakato wa ufunguzi wa vituo vingine vitano katika jiji la Dar es Salaam, hatua inayokuja baada ya ufunguzi wa vituo vingine nchini.

Alisema mbali na Dar es Salaam, Kampuni ya MUNIO ina vituo katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Rukwa pamoja na Mwanza na kwamba mbali na kutoa huduma ya uuzaji wa mafuta, kampuni hiyo imekuwa ikitoa vifaa vya usalama kwa waendesha bodaboda pamoja na kushona sare za madereva na makondakta wa daladala.

Chanzo: habarileo.co.tz