Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Chris Noth ashtumiwa kwa unyanyasaji wa kingono

Big Boyyy Muigizaji Chris Noth ashtumiwa kwa unyanyasaji wa kingono

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wawili wamemshutumu mwigizaji wa Sex And The City Chris Noth kwa kuwanyanyasa kingono mwaka wa 2004 na 2015.

Wanawake hao walitoa maelezo ya kina ya madai ya kushambuliwa kwa The Hollywood Reporter, iliyochapishwa kwa kutumia majina ya bandia Zoe na Lily.

Gazeti hilo linasema wanawake hao hawajuani.

Katika taarifa, Bw Noth, 67, alisema "mahusiano hayo yalikuwa ya maelewano" na kwamba mashtaka ya dhulma za kingono "ni ya uwongo kabisa".

Zoe, ambaye sasa ana umri wa miaka 40, anasema alikuwa na umri wa miaka 22 wakati mwigizaji huyo alipodaiwa kumbaka katika nyumba moja huko West Hollywood mnamo 2004.

Lily, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, anasema alibakwa katika nyumba yake ya Greenwich Village huko New York mnamo 2015 alipokuwa na umri wa miaka 25 na yeye alikuwa na miaka 60.

Nakala ya kina ya mwanahabari Kim Masters pia inawahoji watu kama vile bosi wa Zoe wakati huo, kituo cha matibabu ya ubakaji na rafiki wa Lily ambao simulizi zao zote zinaonekana kuunga mkono madai ya wanawake wote wawili. Nakala hiyo pia inanukuu jumbe za maandishi kati ya Bw Noth na Lily wakati wa madai ya kushambuliwa.

Chris Noth anajulikana kwa majukumu yake ya uigizaji katika Law & Order na Sex And The City, ambapo aliigiza mhusika mkuu, Mr Big.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live