Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muandaaji Tamasha la muziki Uganda ashitakiwa kwa watu kukanyagana Mwaka Mpya

Muandaaji Tamasha La Muziki Uganda Ashitakiwa Kwa Watu Kukanyagana Mwaka Mpya Muandaaji Tamasha la muziki Uganda ashitakiwa kwa watu kukanyagana Mwaka Mpya

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muandaaji wa tamasha la muziki nchini Uganda ameshtakiwa kwa makosa tisa ya uzembe kufuatia vifo vya watu 10 katika mkesha wa mwaka mpya, mjini Kampala.

Abbey Musinguzi alifikishwa mahakamani siku ya Jumanne jioni.

Licha ya kwamba, Bwana Abbey alikanusha mashtaka yote, aliwekwa rumande katika gereza la Luzira.

Muandaaji huyo anadaiwa kusababisha mkanyagano katika eneo la Freedom City Mall alipofunga maduka na kuacha lango moja tu kwa zaidi ya watu 20,000 kutoka.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa siku ya Jumatatu.

Wakili wake anadai mteja wake analengwa kwa sababu anajulikana kuwa mfuasi wa kiongozi wa upinzani wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine.

Wakati huohuo, polisi wamewahoji watu zaidi akiwemo mmiliki wa jengo hilo kurekodi taarifa juu ya tukio hilo baya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live