Dar es Salaam. Mwalimu na mtunzi muziki wa injili nchini Tanzania, Clement Buhembo maarufu Papaa amefariki dunia leo Alhamisi Desemba 12, 2019 katika Hospitali ya Kanisa la African Inland Church (AIC), Makongoro jijini Mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu.
Papaa ni mwalimu maarufu wa kwaya, ambaye alitunga nyimbo kama ‘Chezea pengine, usichezee amani’ inayopatikana kwenye albamu ya Keusi ya kwaya ya Vijana AIC Makongoro, Mwanza.
Umaarufu wa papaa ulianza kufahamika katika albamu ya Kkundu ya kwanza hiyo miaka kadhaa iliyopita.
Papaa ambaye aliokuwa anafundisha kwanza mbalimbali nchini Tanzania, alikuwa pia ni mwalimu wa kwaya ya Vijana Chang’ombe (CVC) ya jijini Dar es Salaam.
Nestory Charles Mtogwa ambaye ni mwanakwaya ya Kwaya ya Vijana Chang’ombe (CVC) amesema Papaa alizidiwa siku ya Jumatatu ya Desemba 9, 2019 alipokuwa akijiandaa na kwaya yake ya AIC Makongoro kwenda kutumbuiza katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza nchini Tanzania.
Amesema baada ya vipimo madaktari walisema alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya nimonia.
Pia Soma
- Mbowe atoa onyo uchaguzi Chadema
- Wapinzani waiongezea CCM ruzuku ya Sh1.1 bilioni
- Malinzi, Mwesigwa walivyotoka gerezani
Papaa akiwa na kwaya ya Vijana Chang’ombe jijini Dar es Salaam ametunga nyingine kama Vunja, Gusa, Badilika, Jihadhari na Mpinga Kristo na albamu ya mwisho ilikuwa inaitwa Pazia la Hekalu.