Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtu anaweza kufikiri Haji ni malaya - Manara

Manara Aibua Gumzo Na Zaylisa, Full Mahaba! Mtu anaweza kufikiri Haji ni malaya - Manara

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, haji Manara amesema kuwa kutokana na mambo anayofanya mitandaoni, mtu anaweza kufikiri kuwa yeye ni malaya kumbe sio kweli.

Manara amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds TV kuhusu maisha yake na kuongeza kuwa, Manara wa mitandaoni ni tofauti na maisha yake binafsi.

"Haji wa social media na Haji real ni vitu viwili tofauti. Mimi naweza kucheza tu na mitandao lakini ki-uhalisia. Mimi sipo kama watu wanavyoniona na huwa sipendi kujielezea acha watu wanihukumu wanavyojua wao lakini mimi na familia yangu na marafiki zangu wanaonijua vizuri au wa karibu wanajua Haji nina tabu kidogo.

"Mfano nikiwa mbele ya kamera naweza kuwa mzungumzaji mzuri sana nje ya hapo tunasafiri au tuko mahali tumekaa unaweza ukakaa masaa mawili hujanisikia naongea na kama sijakuzoea ndio kabisa hutanisikia.

"Watu mtandaoni hawataki tu ile kazi yako unayoifanya, lakini wanataka na kitu gani cha ziada cha kuwauzia bidhaa zao. Mimi ninavyotumia social media kuna mtu anaweza kuona kwamba huyu Haji nitumie jina hili malaya kweli kumbe mimi niko katika drama zangu tu na zinakwenda, zinanisaidia.

"Na ndio maana huwezi kukuta labda baba au mama yangu au ndugu wa karibu au viongozi wangu labda wa Yanga wanapata shida kwa sababu wanajua ninachokifanya na kwamba niko 'smart' kwenye kichwa changu," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live