Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mtu anavyoweza kuchafuliwa kupitia jina lake mtandaoni

Hacker In Mask And Hood Account Hacking 2021 08 26 16 25 33 Utc Scaled 1 1140x640 Mtu anavyoweza kuchafuliwa kupitia jina lake mtandaoni

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upotoshaji kwa kutumia jina ni kitendo cha kutumia jina la mtu, kundi, taasisi au kampuni ambayo si wewe na kulifanya kama lako. Upotoshaji wa jina mara nyingi huwalenga watu, kampuni au taasisi maarufu ili lengo la mpotoshaji litimie kwa urahisi.

Upotoshaji wa jina umekithiri sana katika mitandao ya mbalimbali ya kijamii ambapo ukimtafuta mtu fulani maarufu utaona jina lake linatumiwa na watu wengi.

Sababu za upotoshaji wa jina Upotoshaji wa jina huweza kuwa kwa sababu mbalimbali miongoni mwa hizo ni:

Kujinufaisha au kuingiza kipato - Huu ni upotoshaji wa jina unaohusu zaidi matumizi ya jina la biashara au Kampuni ya kutoa huduma fulani. Mpotoshaji wa jina anatumia jina la Kampuni fulani kama lake Ili aweze kupata wateja wanaopenda kutumia bidhaa halisi za Mwenye jina. Mfano, mtu anaweza kufungua kurasa yenye jina fulani la sabuni pendwa Ili kuwavuta wateja wanaotumia bidhaa hiyo.

Pia, mtu anaweza tumia jina la taasisi fulani ya malipo kuwarubuni watu wafanye malipo kwake ili ajiingizie pesa. Mara nyingi upotoshaji huu kukusudia kutapeli watu

Kuchafua jina la mtu Huu ni utumiaji wa jina la mtu au kampuni kwa lengo la kuharibu jina au heshima yake kwa jamii. Utumiaji huu hufanyika kwa kutumia jina fulani kuweka maudhui au jambo fulani lisilokubaliwa na jamii ili kushusha heshima ya jina husika. Mathalani, mtu anaweza kutumia jina la mtu kuweka maudhui ya ngono, kutusi au jambo lolote la kihalifu.

Kupata Umaarufu Wapotoshaji wa majina wengi wao hulenga kupata Umaarufu kama wa watu waliowaiga majina Yao. Upotoshaji huu hufanyika kwa kutumia jina la mtu maarufu na kuweka maudhui ya mtu huyo ili kuwavuta wafuasi wake.

Upotoshaji huu unawaathiri zaidi Wasanii wa tasnia mbalimbali, ambapo watu hujaribu kutumia majina yao ili kujiongezea wafuasi kutokea kwa mashabiki zao.

Hivyo, ni muhimu sana unapotafuta jina la mtu katika mitandao ya kijamii Kabla ya kuamini, hakikisha akaunti yake ni halisi. Mara nyingi akaunti za watu mashuhuri na taasisi kubwa kuwa na alama ya uthibitisho 'verification badge'

Chanzo: www.tanzaniaweb.live