Akiwa na mwaka 1 tu na siku 152, Ace-Liam Ankrah kutoka Ghana amekuwa mchoraji mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa mujibu wa Rekodi ya Dunia ya Guinness. Ace-Liam, ambaye alianza kupendezwa na sanaa akiwa na umri wa miezi sita, tayari ameunda picha zaidi ya 20.
Hivi karibuni alishiriki katika maonyesho yake ya kwanza kwenye Jumba la Makumbusho la Sayansi na Teknolojia nchini Ghana, ambapo kazi zake 10 za sanaa zilionyeshwa na tisa zikauzwa.
Mama yake Chantelle, anasema aliona mapenzi yake katika uchoraji alipokuwa na umri wa miezi 6 tu. Alikumbuka jinsi alivyounda mchoro wa rangi za kuvutia ulioitwa "The Crawl" alipokuwa akijifunza kutambaa kwenye turubai alilokuwa amemwekea.
Mtoto wako ushagundua Kipaji chake?