Mtoto mmoja ambaye alijifunza mwenyewe kusoma akiwa mdogo amekubaliwa kama mjumbe mwenye umri mdogo zaidi wa taasisi inayotambua watu wenye uwezo wa juu wa akikili- Mensa.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka minne kwa jina Teddy, kutoka eneo la Portishead, Somerset, nchini Uingereza ana weza kuhesabu kuhesabu hadi namnari 100 katika lugha sita zisizo asilia, iliwemo lugha ya Mandarin.
Taasisi ya Mensa huwakubali watu ambao wanapata alama ya asilimia 98 au zaidi kwenye kipimo kilichoidhinishwa cha uwezo wa akili.
Mama yake Teddy, Beth Hobbs, alisema kuwa alijifunza kusoma alipokuwa na umri wa miezi 26 "kwa kutazama televisheni za watoto na kuigiza sauti za herufi ".
Maelezo ya picha, Teddy alikuwa na umri wa miaka mitatu wakati taaisi ya Mensa ilipompatia uanachama. Teddy alikuwa na umri wa miaka mitatu wakati taaisi ya Mensa ilipompatia uanachama.
"Alianza kutafuta herufi na kwahiyo wakati tulipomrejesha katika chekechea baada wa ‘Lockdown’ ya Covid tuliwaambia tulifikiri alikuwa amejifunza mwenyewe jinsi ya kusoama," alisema mama yake.
"Tulipigia simu kutoka shule ya chekechea, ambao walimtuma mwalimu wa darasa la chakechea kumuangalia, ambaye alisema ‘’ndio anaweza kusoma!'"
Mama yake Teddy Beth alisema " huchagua mada inayovutia katika kila baada ya miezi kadhaa, na wakati mwingine huwa ni namba, wakati mwingine huwa ni jeduali la nammba za mara(kusidisha) kwa muda fulani, ambazo zilikuwa ngumu, nchi na ramani, halafu kujifunza kuhesabu katika lugha tofauti"
Ni suala ambalo liliwashangaza sana wazazi wa Teddy.
"Alikuwa anachezea kipakatalishi chake (tablet), akitengeneza sauti hizi ambazo sikuweza kuzitambua , na nikamuuliza zilikuwa nini, na akasema "Mummy, ninahesabu katika lughana ya Mandarin," alisema Bi Hobbs.
Maelezo ya picha, Teddy alijifunza mweneywe kusoma kwa kutazama televisheni za watoto akiwa na umri wa miaka miwili.
Maelezo ya picha, Teddy amejifunza kuhesabu hadi 100 katika lugha sita ambazo sio za asili, mkiwemo lugha ya Mandarin.
Teddy alifanywa kuwa mjumbe wa taasisi ya Mensa wakati alipokuwa na umri wa miaka mitatu, na hivyo kumfanya kuwa mjumbe mwenye umri mdogo zaidi wa shirika hilo nchini Uingereza.
Lakini wazazi wake walisema wanataka akue katika mazingira ya utoto.
"Ameanza kutambua kuwa marafiki zake bado hawawezi kusoma na hajui ni kwanini, lakini ni muhimu sana kwetu kuendelea kumelea," alisema Bi Hobbs.
"Kama anaweza kufanya vitu hivi, nis awa, lakini anaviona kama 'ndio ninaweza kusoma, lakini rafiki zangu wanaweza kukimbia haraka kuliko mimi ', kwahiyo sote tuna vipaji vyetu binafsi."