Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mtoto wa miaka 9 amrekodi baba yake akimshuhsia kipigo mama

Crime Scene 45.jpeg Mtoto wa miaka 9 amrekodi baba yake akimshuhsia kipigo mama

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kiume wa miaka 9 amrekodi video baba yake mzazi akimshambulia vibaya kwa kipigo mama yake mzazi usoni na kichwani kisha mtoto mwingine kuzipigia simu mamlaka za serikali kumripoti baba yao, baba ahakumiwa miaka minne jela.

Tukio limetokea Oktoba 9, 2023 na hukumu imetoka sasa huko Marekani Baba yao alimpiga sana mama yao mzazi kiasi cha kuvuja damu mfululizo.

Wazazi husika wana watoto watatu wenye miaka 15,14 na 9 ambapo mtoto mdogo wa miaka 9 mida ya saa nane za usiku alipoona mama yao anazidi kupigwa na baba yao akaanza kurekodi video isiyopungua dakika sita

Dada yake alipoingilia kati kukinga kwa mikono kumzuia baba yao asimpige mama yao usoni na yeye akapigwa vibao na baba yao, ambapo mtoto mwingine akachukua simu kuzipigia mamlaka za serikali kuwataarifu kinachoendelea nyumbani kwao.

Dakika chache baadaye mamlaka za serikali zikafika na kumkuta baba yao huyo kamkalia juu mama yao ambaye amelala uso ukiangalia sakafuni na damu kumtoka mfululizo.

Baba yao akaanza kujitetea kuwa hajui sababu ya mkewe kuvuja damu. Watoto wao wote watatu walikuwa hapo, Wakati mamlakai zikiendelea na uchunguzi ndio wakagundua mtoto wao mdogo wa mwisho karekodi video ya dakika sita inayoonesha baba yao alichofanya.

Polisi pia wakagundua baba mtu, mama mtu na mtoto wao mmoja wapo wamelewa licha ya mtoto kuwa katika umri usioruhusiwa kulewa (underage). Haraka mamlaka ziliwachukua watoto wote watatu kuwaweka katika uangalizi na malezi salama.

Baba mtu amehukumiwa miaka 4 jela kwa makosa kadhaa yakiwemo ya unyanyasaji/ukatili, kumpiga mzazi mwenzie mbele ya watoto, na kutokuwa na malezi mazuri kwa watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live