Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Shah Rukh Khan hali tete

Aryan Khan Mtoto wa Shah Rukh Khan hali tete

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Aryan Khan (23) mtoto wa nyota wa filamu za Bollywood Shah Rukh Khan, ataendelea kusota jela baada ya kukosa dhamana kutoka Mahama maalum ya mjini Mumbai nchini India kutokana na msala wake wa dawa za kulevya unaomkabili.

Submitted by William Shemoka on Ijumaa , 15th Oct , 2021 Picha ya Aryan Khan mtoto wa nyota wa filamu za Bollywood Shah Rukh Khan akiwa na Maafisa wa NCB

Mtoto huyo alikamatwa kwa kuhusishwa kwenye tukio ambalo dawa za kulevya zilipatikana kwenye meli iliyokuwa ikielekea pwani ya Mombai ambapo taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya NCB inadai kuwa Aryan alikuwa mtumiaji wa kawaida wa dawa zilizozuiliwa na Taifa hilo kwa miaka kadhaa.

Sasa Aryan atalazimika kukaa jela mpaka Oktoba 20 kutokana na Mahakama Kuu na Vikao vya Mahakama kufungwa kuanzia Oktoba 15 - 19 kwa sababu ya sikukuu ya Dussehra.

Chanzo: eatv.tv