Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Prof Jay, Wa Babalevo Watusua

Baba Levo Prof Jay Mtoto wa Prof Jay, Wa Babalevo Watusua

Tue, 18 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FAMILIA za mastaa wawili Bongo Profesa Jay na Baba Levo zimegubikwa na furaha baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka na watoto wao kung’ara kwa kupata daraja la kwanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Profesa Jay amempongeza binti yake huyo kwa kuandika;

“Matokeo Form Four. Lisa Joseph Haule –division one point 10. Congratulations to my beautiful daughter @l.i.s.a.h_profjize. Safari ndiyo kwanza inaanza, keep your head up. Pia hongera sana mama mzaa chema @mke_ wa_profjize kwa miongozo na malezi bora kwa mwanetu…”

Kwa upande wa Baba Levo, pamoja na mwanawe Levo kufanikiwa kupata division one ya pointi 9 katika matokeo ya kidato cha pili, lakini amesema hampi zawadi mpaka apate division one ya pointi 7.

Huwa Sipendi Ubishi....!! Haya mkeka Huo Apo ...! Au Nendeni wenyewe Kwenye Web Ya Necta Chagua MAKONGO SECONDARY Jina Revocatus Clayton???????????????????? One Ya Tisa Na Hapati Chochote...!!!!!Nataka One Ya Saba...!!???????????? 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live