Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Mr Ibu abadili jina la Baba yake

Mtoto Wa Mr Ibu Abadili Jina La Baba Yake Mtoto wa Mr Ibu abadili jina la Baba yake

Sun, 3 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimepita saa chache tangu kutoka taarifa ya kifo cha muigizaji kutoka Nigeria, John Okafor, maarufu ‘Mr Ibu’, sintofahamu imeibuka mitandaoni baada ya mtoto wa kike wa kuasili wa msanii huyo aitwaye Jasmine Okekeagwu, kubadili jina kwenye akaunti ya TikTok ya Mr Ibu na kuandika jina lake.

Mtoto huyo si mtoto wa damu wa Mr Ibu, bali alilelewa na mwigizaji huyo, akaunti aliyobadili ina wafuasi milioni 1.3, sasa ameweka jina lake Lady Jasminec. Kitendo hicho kimezua mijadala kwenye mitandao huku wengi wakionesha kuchukizwa na nacho na kudai siyo cha kiungwana.

Ikumbukwe kuwa Januari mwaka huu, Onyeabuchi Okafor ambaye ni mtoto wa kiume wa Mr Ibu na Jasmine mtoto wa kuasili, walidakwa na polisi nchini humo kwa madai ya kuiba fedha zilizokuwa zimewekwa kwa ajili ya matibabu ya muigizaji huyo.

Watoto hao walidaiwa kuingia kwenye mifumo ya benki kwa kutumia simu ya muigizaji huyo waliyokuwa wakiimiliki na kuiba #Naira 55 milioni ambazo ni zaidi ya Sh88.3 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live