Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Mobeto ampa laana Diamond

Diamond DYLAN Hamisa.png Mtoto wa Mobeto ampa laana Diamond

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dyllan; ni mtoto wa mastaa wawili wakubwa nchini Tanzania, Diamond Platnumz na Hamisa Mobeto ambaye anadaiwa kumpa laana baba yake huyo.

Hii ni baada ya kusemekana kwamba, tofauti na wanawe wengine, lakini yeye Diamond na familia yake wanambagua.

Inafahamika Diamond au Mondi ana watoto wanne; wawili amezaa na Zari The Boss Lady waitwao Tiffah Dangote na Prince Nillan, mwingine amezaa na Hamisa aitwaye Dyllan kisha akazaa Tanasha Donna mtoto anaitwa Naseeb Junior (NJ).

Diamond amekuwa akiwaonesha watoto watatu upendo wa hali ya juu pamoja na kwamba wapo nje ya nchi kwa maana ya Afrika Kusini na Kenya, lakini ameshindwa kufanya hivyo kwa Dyllan ambaye yupo hapahapa nchini Tanzania tena wote wanaishi Mbezi-Beach jijini Dar.

Hayo yote yanakuja siku chache baada ya Diamond kuungana na familia yake kumtakia heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa mwanawe aliyezaa na Tanasha kutoka nchini Kenya.

Diamond na familia yake walionesha walionesha mapenzi tele wakimtakia kheri ya siku ya kuzaliwa pamoja na baba yake ambaye ni Diamond.

Siku za hivi karibuni ilikuwa ni birthday ya Dyllan wa Hamisa ambapo mtoto huyo alishuhudiwa akiisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa upweke wa hali ya juu huku familia yote ya Diamond wakiwa nchini Afrika Kusini kusherehekea birthday ya Tiffah Dangote.

Kuna wanaosena Diamond na familia yake kutomjali Dyllan ni kawaida na haina maana mbaya na kuna wanaosema haipendezi kwani wanamuachia upweke mtoto wao na wanakuwa kama wamemtenga kwani anaona wenzake wanavyofanyiwa hivyo itakuwa ni laana kubwa kwa staa huyo.

Hata hivyo, akizungumza na Gazeti la IJUMAA hivi karibuni, Hamisa alisema kuwa, Diamond amesitisha kutoa matumizi kwa mtoto huyo na ameshika jukumu la malezi yeye mwenyewe kama singo mama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live