Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Masogange: Natamani kuwa muigizaji kama mama

Sania Na Mama Yake Mtoto wa Masogange: Natamani kuwa muigizaji kama mama

Sat, 27 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa aliyekuwa video vixen maarufu Bongo Agness Masogange, Sania Sabri, ameibuka na kusema anatamani kuja kuwa muigizaji kama mama yake.

Mbali na kazi hiyo, Sania amesema anatamani pia kuwa mhasibu na ndio masomo aliyoyachagua shule hivyo akimaliza kidato cha nne baadaye mwaka huu, ataendelea kujibidiisha katika masomo ya uhasibu hapo baadaye.

“Ndio natamani kuwa kama mama. Lakini pia natamani kuwa mhasibu nikae kwenye kiti cha kuzunguka hivi,” alisema Sania.

Masogange aliyekuwa akitikisa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata alifariki dunia Aprili 20, 2018 katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar alikolazwa kwa siku nne akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia (Nimonia).

Mwili wake ulipumzishwa kijijini kwao Utengule jijini Mbeya baada ya kuagwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

Mrembo huyo aliyeonekana kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva kama Masogange ya Belle 9, Msambinungwa ya Tundaman na nyinginezo ameacha mtoto huyo mmoja pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live