Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Kanye aandaa albamu

Kanye West North Mtoto wa Kanye aandaa albamu

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mkubwa wa kike wa Kanye West na Kim Kardashian "North West" anaendelea kufuata nyayo za Baba yake kwani na yeye ameanza rasmi safari yake ya muziki kwa kutangaza kuwa yupo katika maandalizi ya Album yake ya kwanza ambayo ameipa jina la "Elementary School Dropout"

"I’ve been working on an album.....and it’s called Elementary School Dropout.”---North West ameongea kauli hii Jumapili kwenye "Listening Party" ya Album ya Kanye West na Ty Dolla Sign "Vultures" Phoenix Marekani.

Jina la Album ya North West limeendana kidogo na jina la Album ya kwanza ya Kanye West iliyotoka mwaka 2004 "The College Dropout".

Kabla ya North West Weekend hii kutangaza kuwa yupo katika maandalizi ya Album, mwezi mmoja uliopita Kanye West na North West walitoa Collabo yao ya kwanza "Talking / Once Again” ambayo iliingia kwenye Chart za Billboard Hot 100 na ikashika nafasi ya 30, hali hii ilipelekea North West awe miongoni mwa wasanii wenye umri mdogo zaidi kuwahi kuingiza nyimbo zao kwenye Chart za Billboard.

North West alizaliwa mwaka 2013, mpaka sasa ana umri wa miaka 10, mara kadhaa amekuwa akifunguka kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa Mwanamuziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live