Ukiambiwa mapenzi ni upofu usiwe unabisha! Bila shaka unamfahamu Bill Gates, yule bilionea mkubwa anayeshika namba sita duniani akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 104 za Kimarekani.
Bill Gates anao watoto watatu, Rory Gates, Jennifer Gates na Phoebe Gates ambaye ndiye mwanaye wa mwisho! Sasa unaambiwa kitindamimba huyu wa Bill Gates, ame-make headline kwenye vyombo vikubwa vya habari duniani, baada ya kumtangaza rasmi mpenzi wake!
Kilichowashtua wengi, ni asili ya mwanaume huyo. Jina lake kamili anaitwa Robert Ross, Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika! Unaambiwa mtoto wa Bill Gates hapa kafa kaoza, hasikii wala haambiwi, amezama kwenye penzi la mwamba!
Pengine kwa utajiri wa baba yake, wengi walitarajia Phoebe awe kwenye uhusiano wa kimapenzi au pengine aolewe na mtoto wa bilionea mwingine duniani, au mtu mashuhuri ambaye anakaribiana na levo za familia yake lakini hali ni tofauti!
Ameudhihirishia ulimwengu kwamba mapenzi hayachagui rangi, kabila, dini, utajiri wala umaskini.
Pengine una shauku kubwa ya kutaka kumjua kwa undani mwamba huyu aliyeuteka moyo wa binti wa bilionea! Siyo kinyonge, jamaa amewahi kufanya kazi kwenye Kampuni ya Google akiwa kama Meneja wa Bidhaa na sasa amefungua kampuni yake ya kiteknolojia iitwayo Lume.
Amepiga shule, anazo digrii mbili za masuala ya teknolojia ya mawasilianoalizozipatia katika Chuo Kikuu cha Standford University ambako ndiko alikokutana na mrembo huyo! Lakini pia jamaa ni msanii wa muziki.