Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Beyonce kusikika kwenye Animation ya "The Lion King"

Beyonce , Ivy Mtoto wa Beyonce kusikika kwenye Animation ya "The Lion King"

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Beyonce, Blue Ivy (11) ameripotiwa kuwa sauti yake itatumiaka kwa mara ya kwanza katika filamu (animation) ya ‘Mufasa: The Lion King’ akiungana na mama yake ambaye tayari alishapewa uhusika toka hapo awali.

Katika filamu hiyo Blue ataweka sauti ya binti Simba aitwaye Kaira huku mama yake akiigiza sauti ya mke wa Simba ambapo animation hiyo inatarajiwa kutoka Desemba 20, 2024.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Beyonce kufanya kazi pamoja na binti yake, ikumbukwe kuwa mwaka Jana Blue alizunguka na Mama yake katika ziara ya ‘Renaissance’ akiwa kama kiongozi wa dancer.

Blue Ivy, ni mtoto mkubwa wa Beyonce ambaye amempata na msanii Jay-Z.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live