Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto arudishwa Tanzania baada ya Wazazi wake kukamatwa na Dawa za kulevya China

Fri, 23 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Taarifa tuliyoipokea kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ni kuhusu Watanzania wawili wamekamatwa nchini China January 19, 2018 wakiwa wamemeza dawa za kulevya tumbo kwenye uwanja wa ndege wa Baiyun Guangzhou.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupamba na Dawa za Kulevya nchini Rogers Siang’a watuhumiwa hao ni Baraka S. Malali na Mkewe Ashura H. Musa wamekamatwa wakiwa na Mtoto wao mdogo mwenye umri wa miaka 2 na miezi 9.

Kamishna Siang’a amesema baada ya kukamatwa  walihifadhiwa kwenye chumba maalum kwa muda ndipo Baraka alitoa Pipi 47 kwa njia ya haja kubwa, huku Ashura akitoa Pipi 82.

Siang’a amesema Serikali ya China iliwasiliana na Serikali ya Tanzania kuhusiana na suala la Mtoto huyo, ambapo walikubaliana kumrudisha mtoto huyo nchini. Mamlaka ya kupambana na Dawa za Kulevya ikishirikiana na Ustawi wa Jamii inafanya jitihada za kuwasiliana na ndugu wa watuhumiwa ili kuhakikisha mtoto huyo anakabidhiwa kwa ndugu zake ili apate matunzo.



“MPAKA WAUZA DAWA ZA KULEVYA WANASEMA VYUMA VIMEKAZA” -ROGERS SIANG’A

Chanzo: millardayo.com