Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mtoto aliyevunja rekodi ya dunia kwa kuzaliwa kabla ya umri sahihi

XBYEENSYRBHVLG26LZJLQZCQF4 Mtoto aliyevunja rekodi ya dunia kwa kuzaliwa kabla ya umri sahihi

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto Curtis Means kutoka nchini Marekani amevunja rekodi ya maajabu duniani inayotolewa na Guiness kwa kuzaliwa akiwa na wiki 21 na siku na anatajwa kuwa ndiye mtoto mchanga zaidi duniani kuzaliwa kabla ya muda wake.

Curtis Means alizaliwa Birmingham, Alabama, mwaka jana akiwa na uzani wa gramu 420 (14.8 ounces).

Rekodi ya Guinness World imethibitisha kuwa Curtis, ambaye sasa ana umri wa miezi 16 ameweka rekodi mpya.

Ujauzito wa kawaida hudumu kwa wiki 40 hadi mtoto anapozaliwa, kumaanisha Curtis aliyezaliwa akiwa na wiki 19 ndiye mtoto mchanga zaidi kuzaliwa kabla siku yake.

Mama yake, Michelle Butler, alipata uchungu wa uzazi na kupelekwa hospitali Julai 4, 2020 usiku wa tafrija za sherehe za uhuru.

Alijifungua mapacha, Curtis na C'Asya,wakati wa chakula cha mchanasiku iliyofuata.

C'Asya alifarikki siku moja baadaye. Hospitali ilisema huwa inawapatia wazazi msaada maalum katika mazingira kama hayo , kuwaruhusi kuwabeba watoto wao wachanga japo kwa muda kidogo ambao huenda watakua pamoja.

Lakini akiwa na chini ya asilimia moja ya kunusurika kifo, Curtis aliponea katika chumba cha uangalizi maalum.

Alitolewa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua baada ya miezi mitatu na kuruhusiwa kwenda nyumbani mwezi Arili mwaka huu baada ya kulazwa hospitali kwa siku 275.

Madaktari wa tiba ilibidi wamsaidie kujifunza jinsi ya kupumua na kutumia kinywa chake kula.

Bi Butler, wa kijiji cha Eutaw, huko Alabama, alisema katika taarifa: "Kuweza hatimaye kumpeleka Curtis nyumbani na kuwashangaza watoto wangu wakubwa na kaka yao mdogo ni wakati ambao nitakumbuka daima."

Curtis - ambaye ana ndugu wakubwa watatu - bado anahitaji oksijeni ya ziada na bomba la kulisha, lakini madaktari wanasema yuko katika afya njema.

Dk Brian Sims, Chuo Kikuu cha Alabama huko Birmingham mtaalamu ambaye alisimamia kuzaliwa kwakei, aliiambia Guinness World Records:"Nimekuwa nikifanya hivi karibu miaka 20, lakini sijawahi kuona mtoto mchanga kama huyu akiwa na nguvu kama alivyokuwa. Curtis alikua na kitu maalum.

Curtis alivuka kwa saa 24 rekodi za awali,ambayo ilikuwa ikishikiliwa na mtoto Richard Hutchinson wa Wisconsin, ambaye alizaliwa akiwa na wiki 21 na siku mbili.

Kabla ya Richard,rekodi hiyo ilisalia bila kuvunjwa kwa miaka 34, na ilikuwa ikishikiliwa na mtoto wa kiume aliyezaliwa Ottawa, Canada, akiwa na wiki 21 na siku tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live