Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto alieshinda Beti, Baba azikataa Pesa

Dogo Beti Mtoto alieshinda Beti, Baba azikataa Pesa

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 amebaki kwenye njia panda baada ya kushinda hela ndefu kutoka kwenye mchezo wa Kamari (betting) lakini babake akazikataa hela hizo kwenye nyumba yake.

Kulingana na taarifa kutoka majarida ya Nigeria ambayo yalipata kisa hicho baada ya ndugu wa kijana huyo kuulizia msaada wa kimawazo mitandaoni, kijana huyo alikuwa ameweka ‘mkeka’ kwenye Kamari ya mitandaoni akitumia Naira 450 ambacho ni sawa na TSh. 2,000 na alishinda TSh. Milioni 188.

Kwa furaha alikimbia nyumbani na kuwataarifu wazazi wake, lakini baba mtu alikataa kumsikiliza akisema kuwa hawezi kuidhinisha pesa hizo katika nyumba yake, licha ya kuoneshwa pesa nyingi alizoshinda.

Aliyeripoti taarifa hii ambaye ni Kaka wa kijana huyo amesema, baba anazikataa pesa wakati Kodi ya nyumba yao inamalizika miezi miwili ijayo!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live