Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mtiti mzito kati ya Angelina Jolie na Brad Pitt juu ya umiliki wa mali

Edtdy.png Angelina Jollie akiwa na mtalaka wake Brad Pitt's

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Mchakato wa Talaka kati ya nyota wa filamu duniani Angelina Jolie na mume wake Brad Pitt's kukamilika mwaka 2019, bado wawili hao wapo kwenye mzozo wa umiliki wa mali za kifahari zilizopo katika mji wa Miraval nchini ufaransa.

Malalamiko juu ya umiliki wa mali yali wasilishwa na Brad huku akimshutumu nyota huyo wa filamu kwa kujaribu kupunguza hisa zake kutoka asilimia 60 hadi 50 katika eneo hilo lenye hekari 1000 ambalo lina thamani ya dola milioni 164 sawa na shilingi bilioni 380.316 za kitanzania.



Mjengo wa kifahari wanaomiliki wawili hao nchini Ufaransa.

Aidha inaelezwa kuwa Mali hizo zipo chini ya mashirika tofauti tofauti ambayo yanadhibiti kwa mujibu wa maelekezo ya Mahakama, yanayoeleza kuwa mali hizo zinamilikiwa na kampuni ya bwana Brad ya Quimicum yenye hisa ya asilimia 60 ambazo zipo chini ya uangalizi wa kampuni yake nyingine ndogo ya 'Mondo Bongo' huku Angelina akiwa na hisa za asilimia 40 kupitia kampuni yake ya Nouvel.

"kwa miaka minne iliyopita, kampuni ya Nouvel ya Angelina haikuitendea haki kampuni ya Quimicum kwa kuchelewsha kwa makusudi taratibu za awali za malipo ya kila mwaka ikiwa nipamoja na kumbadilisha meneja anaesimamia mali hizo" imesema taarifa ya Mahakamani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live