Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtifuano wa H.Baba na Mwijaku wafikia pabaya

Mwijaku12 H Baba Mtifuano wa H.Baba na Mwijaku wafikia pabaya

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kudai kujitenga kumshabikia msanii Harmonize, mkongwe wa Bongo Fleva, Hamisi Ramadhani Baba (H Baba) na mtangazaji Burton Mwemba almaaarufu Mwijaku wameingia kwenye vita nzito ya kuvuana nguo. H Baba anadai kwamba, Mwijaku amekuwa akitengeneza sauti zake kuhusu kujitenga kwake na Harmonize au Konde Gang kwa lengo la kumchafua.

H-Baba anasema kuwa, Mwijaku anajaribu kumgonganisha na Harmonize, lakini kwa upande wake hajaingia popote wala hajatoka popote baina ya Konde Gang ya Harmonize na WCB ya Diamond kwani alidaiwa kuhamia huko.

“Mimi sijawahi kujitoa sehemu yoyote na pia sijaenda sehemu yoyote. Ndugu yangu yule (Mwijaku) anatakiwa atulie na atuache mimi na Harmonize tumetoka mbali. “Wakati tunapambana vita yetu sisi wawili yeye hakuwepo. Kwa hiyo ndugu Mwijaku kuwa makini sana,” anasema H Baba.

Kwa upande wake, Mwijaku au DC wa Instagram ameibuka na kuweka wazi kuhusu maneno ya msanii H Baba aliyomwonya kuwa makini kutokana na taarifa anazozisambaza kwamba Harmonize na H Baba wamevuruga urafiki baada ya H Baba kum-unfollow Konde Boy kwenye Instagram.

Mapema Februari 15, H Baba, katika mahojiano na kituo kimoja cha habari alisema kwamba yeye na Harmonize ni marafiki wa kitambo na katu hakuna mtu anayeweza kuwachonganisha na kumuomba Mwijaku kukaa mbali na urafiki wao huo.

Mwijaku amemwambia H Baba kwamba Konde Gang hawana haja na yeye kwani walifanya kumpunguza tu kutokana na ukongwe wake.

Ugomvi wa wawili hao umekuwa kwa zaidi ya wiki moja sasa baada ya H Baba kuposti picha na video za Diamond huku akimpongeza kutokana na ufanisi wake mkubwa wa kuwa mwanamuziki mkubwa barani Afrika. Hapo ndipo mtangazaji Mwijaku alipoanza kumkejeli na kusema kwamba anajigonga kwa Diamond ili apewe dili Wasafi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live