Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtasubiri ya Diamond na Zuchu hewani kama kawa

DIAMOND HDJSK Diamond na Zuchu

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtasubiri; ni video matata ya wimbo namba nane kwenye EP ya FOA ya Diamond Platnumz aliyomshirkisha msanii wake Zuchu ambayo pamoja na kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), bado kitu kinaendelea kupepea hewani kama kawa pale mjini YouTube.

Kufuatia ishu hiyo, baadhi ya watu wanajiuliza lile tangazo la kufungiwa limekaaje kama mzigo bado unapeta hewani ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni kumi?

Taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo ilieleza kuwa TCRA ilipokea taarifa kutoka Basata ya kuzuia usambazaji wa video ya wimbo wa wasanii hao unaopigwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya utangazaji.

Ilisema sababu za kuzuia video hiyo ni kutokana na kuwa na kipande kinachoonesha wahusika wapo kanisani wanaimba kwaya, lakini baadaye wakaacha na kuelekea kwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live