Mtangazaji wa Televisheni wa Uingereza Michael Mosley, amepatikana leo akiwa amekufa Kisiwani Symi nchini Ugiriki siku nne baada ya kupotea.
Daktari huyo wa televisheni na mwanaharakati wa maisha ya afya alikuwa mtu mashuhuri kwenye televisheni kwa takribani miaka 20.
Mosley (67), alikuwa mapumzikoni kisiwani humo pamoja na mke wake, hata hivyo Jumatano iliyopita alikwenda peke yake kutembea ndani ya kisiwa hicho chenye mawe na miamba mingi.
Mwili wake ulikutwa kwenye mawe karibu na bahari na baa iliyopo ufukweni. Polisi wamesema hakuna dalili yoyote ya uhalifu na bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
Uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.