Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Msoma habari anayetumia akili bandia aanza kazi

Fedha Kuwait Msoma habari anayetumia akili bandia aanza kazi

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Habari la Kuwait News, limemtambulisha mtangazaji wake wa kwanza mwenye muonekano wa kike aliyetokana na Teknolojia ya akili bandia (Artificial Intelligence), ameanza kuonekana kwenye habari za Kuwait wikiendi iliyopita.

Kupitia mtandao wa Twitter, Shirika la habari la Kuwait News liliposti video iliyomuonyesha mwanahabari huyo aliyetengenezwa kwa Kompyuta akijitambulisha kwa jina la Fedha.

Licha ya kuonekana akifanana kama binadamu wa kawaida kuanzia mwonekano, matamshi na mijongeo ya mwili, Fedha si binadamu halisi bali ni picha jongevu iliyoundwa kwa AI, ikiwa na sifa zote za binadamu.



"Mimi naitwa Fedha, mtangazaji wa kwanza nchini Kuwait ninayefanya kazi kwa kutumia akili bandia kupitia teknoloji aya Artificial Intelligence katika Shirika la Kuwait News.

"Habari za aina gani mnapendelea? Ngoja tusikie maoni yenu," alisema kwa lugha ya Kiarabu.

Abdullah Boftain, Mhariri Mkuu Msaidizi wa Shirika la Kuwait News, ameliambia Shirikala Habari la AFP kwamba wamekuja na ubunifu huo mpya kwa lengo la kuboresha huduma zao za utoaji wa habari.

Boftain amesema kwa sasa wanamfundisha Fedha lafudhi ya Kuwait na siku chache zijazo, ataanza kusoma taarifa ya habari runingani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live