Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msizwa: Sijampa talaka Esma

Msizwa Na Esmaa Msizwa: Sijampa talaka Esma

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Msizwa amefunguka kuwa, licha ya kwamba wameshaachana na aliyekuwa mkewe dada wa Diamond, Esma Khan, bado hajampa talaka.

Akizungumza na televisheni za mitandaoni hivi karibuni, Msizwa alisema, yeye alikuwa serious na ndoa hiyo licha ya kwamba Esma ndiye aliyomfata kuomba amuoe na kweli alifanya hivyo lakini Esma amekuwa akizungumza mambo tofauti kwa jamii.

“Anasema kwamba mimi nilimuoa ili nipate umaarufu jambo ambalo si la kweli, alinifuata kuniomba nimstiri na kweli mimi nikamstiri lakini baadaye akatoka, sijampa talaka mpaka sasa,” alisema Msizwa.

Ndoa ya wawili hao ilikuwa na kishindo kikubwa mjini ambapo mastaa mbalimbali walihudhuria akiwemo Diamond Platnumz lakini hata hivyo haikudumu muda mrefu ikaota mbawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live