Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msizwa: Esma ndio alinitongoza

Msizwa Na Esma Msizwa: Esma ndio alinitongoza

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mume wa Esma Platnumz, Msizwa ameweka plain kwamba, dada huyo wa Diamond ndiye aliyeomba mahusiano naye kabla ya kufunga ndoa na kuvunjika ndani ya miezi mitatu.

Msizwa amefunguka hayo alipofanya mahojiano na moja ya televisheni za mitandaoni ambapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano yake.

Alisema, Esma ndiye aliyemuanza yeye na akamkubalia lakini hata hivyo yeye ndiye alikuwa chanzo cha ndoa hiyo kuvunjika.

“Niwaambie hii sijawahi kuisema mahali popote. Yeye ndiye alinitongoza na sio mimi nilimtongoza,” alisema Msizwa.

Jamaa huyo ambaye ni mfanyabishara maarufu mjini, amesema Esma ndiye alikuwa na matatizo maana kabla ya kumuoa yeye, tayari alikuwa na wake wawili ambao anao mpaka leo.

“Mke wangu wa kwanza tuna miakia 13, wa pili tuna miaka saba sasa hapo utaona nani alikuwa na tatizo,” alisema Msizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live