Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msinisahau, nipeni hata kolabo, nimewasaidia sana - Lukamba

Lukamba Diamond Rayvanny Msinisahau, nipeni hata kolabo, nimewasaidia sana - Lukamba

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Lukamba amewakumbusha fadhila zote alizowai kuwafanyia Wasanii wakubwa kabla ya kupata mafanikio walionayo kwenye muziki.

Lukash ambaye amewahi kuwa mpiga picha wa Diamond amesema lengo ni kuwakumbusha wasanii hao wasimsahau na wakubali kushirikishwa kwenye kazi zake ili aweze kupata kipato kikubwa kupitia muziki kama wao.

Amesema, Rayvanny amemsaidia sana hivyo hawezi kumnyenyekea sana kuomba kolabo, naye Harmonize amekula sana elfu mbili mbili zake lakini kwa sasa amem-block

Lukamba ameongeza kuwa Zuchu amepanda sana gari lake aina ya Altezza, Lavalava naye alimrekodia video yake ya kwanza hadi Diamond akamuona.

Aidha, Lukamba amedai kuwa Whozu naye alikuwa akimuomba 'ampostie' vichekesho vyake hadi akamfanya kuwa maarufu.

hajaishia hapo, Lukawise ameongeza kuwa aliyewahi kuwa bosi wake, Diamond Platnumz amlimtengezea video nyingi sana nzuri na za kibunifu hadi amekuwa maarufu zaidi Afrika na Duniani.

Una maoni gani kuhusu kauli hii ya Lukamba?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live