Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msiniletee U-team wenu kwa watoto wangu- Diamond Platnumz

10231 Zassaqewassas TZW

Thu, 28 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii Diamond Platnumz bado anazidi kugonga vichwa vya habari na wanae watatu.



Muimbaji huyo kutokea WCB amesema habagui watoto wake na wala hapendi mambo ya utimu. Kupitia Instagram ameweka picha akiwa na mwanae Daylan na kuandika;

“His is my Kid and he will forever be my Kid, tena My Beloved Kid, na si vinginevyo. Halafu cha kuongeza, msiniletee U-team wenu kwa watoto wangu! they are all my Kids, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yeyote,” ameeleza Diamond.

Diamond Platnumz ni baba wa watoto watatu, watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’ akiwa amezaa na Zari The Boss Lady na mtoto wa mwisho, Daylan akiwa amezaa na Hamisa Mobetto.

Kufuatia kitendo cha Hamisa Mobetto kuzaa na Diamond wakati muimbaji huyo bado alikuwa na mahusiano na Zari ndicho kilipelekea warembo hao kuanza kurushiana maneno mitandaoni kitu kilichokuja kuzaa kile kinachoitwa team Hamisa na team Zari.

Loading...
Chanzo: bongo5.com