Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimu wa Krismas: Zari na wanae watokelezeaa na sare ya vitenge

Mdksl Zari Zari na wanae

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mipango imepamba moto kuelekea sherehe za siku kuu za krismas wiki mbili zijazo na familia mbalimbali za wetu wenye ‘nacho’ zinazidi kufanya maandalizi kabambe.

Familia ya mwanasosholaiti Zari Hassan haijaachwa nyuma katika hili kwani wametokea kwenye video moja ya TikTok wakiwa wamepiga pamba moja safi.

Zari alipakia video hiyo fupi ikimuonesha akiwa na familia yake nzima kwa maana ya wanake watano ambao wote walitokea na sare ya vitengo vya rangi nyekundu kama mashuka ya Kimaasai.

Walikuwa kwenye chumba komja cha kifahari huku wakipigwa picha na Zari alichapisha maneno kwenye video hiyo akisema kuwa familia ndio kila kitu juu chini.

Video hiyo ambayo imetazamwa na watu wengi iliwafurahisha watumizi wa TikTok ambao hawakuchelewa kumwaga furaha yao na kumsifia Zari jinsi anaiweka familia yake karibu licha ya mishe nyingi na umaarufu mitandaoni.

“Mama mrembo na wapendwa wake  hili ndilo jambo la muhimu mwisho wa siku,” mmoja aliandika.

“Aki wew ni mrembo! unaonekana kama wewe ndio dada Yao. sijui mama yenu Yuko wapi hapo,” mwingine alitania kutokana na kwamba mjasiriamali huyo licha ya umri kusonga, bado urembo wake ni mbichi.

“Mashallah yarabi napenda jinsi unavyoipenda familia yako, Mwenyezi Mungu akubariki daima,” Shira FK alisema.

Wengine walisifia jinsi watoto wake wa kwanza watatu ambao ni watu wazima wanavyojiweka mbali na sakata lake la mitandaoni na mpenzi wake Shakib Cham ambaye amekuwa akisemekana ni kibenten tu.

“Napenda vijana wako wakubwa jinsi wanajiweka mbali na mitikasi yako, hiyo ndio heshima kwa mzazi,” mmoja alisema.

“Siamini hivi karibuni Tiffah na Nillan watakuwa warefu kuliko mama pia, familia yenye furaha zaidi kheri njema ya msimu wa sikukuu za krismas,” mwingine alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live