Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimu mpya wa Big Brother Nigeria waanza kwa kishindo

Msimu Mpya Wa Big Brother Nigeria.jpeg Msimu mpya wa Big Brother Nigeria waanza kwa kishindo

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa saba wa shindano la Big Brother Nigeria (BBNaija), limeanza kushika kasi baada ya kuzinduliwa rasmi Julai 23, 2022 ambapo mastaa 12 wa nchini humo watachuana kutafuta mshindi.

Mashindano hayo yanaoneshwa moja kwa moja na DSTV Chaneli namba 198 na 199 ambapo mashabiki kutoka kona zote za Bara la Afrika, watakuwa wakishuhudia kila kinachoendelea kwenye mjengo huo.

Mastaa 12 walioingia kwenye shindano hilo ni pamoja na Amaka, Beauty, Bryann na Christy O. Wengine ni Cyph, Groovy, Daniella, Ilebaye, Kess, Khalid, Pharmsavi na Phyna ambao wote ni mastaa, kila mmoja akiwa na ‘swaga’ za kipekee.

Unaweza pia kufuatilia kila kinachoendela mjengoni kwa kupitia website na mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live