Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimchukulie Poa Hamisa

Mobeto Pic Data Msimchukulie Poa Hamisa

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAARIFA ikufikie kwamba, kabati la mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Hamisa Mobeto limejaa tuzo za Bongo na kimataifa. Hamisa alianza kutwaa Tuzo ya Miss XXL, After School Bash mwaka 2010.

Mwaka 2011 aliibuka Mshindi wa Pili wa Miss Dar Indian Ocean, Mshindi wa Pili wa Miss Kinondoni na aliingia Nusu Fainali ya Miss Tanzania 2011 ambapo Genevieve Mpangala aliyetwa taji hilo.

Mwaka 2012 alishiriki Miss Universe Afrika na kuingia kwenye orodha ya warembo 10 bora.

Kwa miaka miwili mfululizo Hamisa alitajwa kwenye Tuzo za Starqt Awards ambazo hutolewa nchini Afrika Kusini.

Mwaka 2016 alishinda Tuzo ya Abryanz Style Fashion (ASFA2016) jijini Kampala, Uganda katika kipengele cha Fashionista of The Year Award East Africa.

Mwaka 2017 alishinda Tuzo ya People Choice Awards katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo uliofanyika Bedford View City Hall, Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mwaka 2021 ametwaa Tuzo ya Scream kutoka Nigeria ambayo hutolewa kwa vijana mbalimbali barani Afrika waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali. Pia mwaka 2021 ametwaa Tuzo ya Mshawishi Bora wa Chapa wa Mwaka (Brand Influencer of the Year).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live