Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msichana achoma cheti chake cha digrii kwa kukosa kazi

PICHAAAAAAA Msichana achoma cheti chake cha digrii kwa kukosa kazi

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binti mmoja anayejulikana kama Bridget Thapwile Soko msomi wa shahada ya Biashara nchini Malawi amewaacha watu hoi baada ya kuteketeza cheti chake cha elimu kwa madai anayosema kuwa haikumsaidia na kitu chochote.

Bridget amedai kuwa alichanganyikiwa alishindwa kupata kazi miaka minne baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Exploits lililoko Malawi akisema ni bora aichome shahada hiyo na kuweka cheti cha ndoa yake.

Katika video iliyosambaa kwenye mtandao wa TikTok, mwanadada huyo aliimba na kumdhihaki kila mtu ambaye alishindwa kumtolea nafasi za kazi au hata kumwalika kumhoji kuhusu kazi.

Sauti za watu walioshuhudia tukio hilo mwanamke akichoma cheti zilisikika wakishtuka na kujaribu kumshauri aghairi hatua yake ila hakuambilika wala kusemezeka.

Usimamizi wa chuo kikuu cha Exploits ulilaani kitendo chake pindi tu walipoona video hiyo huku wakisema kitendo hicho ni kama cha kudhihaki shule hiyo.

“Kulingana na tunavyojijazia, msichana huyo alifanya hivi ili kukidhihaki chuo cha Exploits na kuchafua sifa ya chuo kikuu.''

“Kwa hivyo chuo kikuu kinabatilisha shahada ya usimamizi wa biashara uliyopewa. Msimamizi wa shule hiyo alisema.

"Kwa hivyo, wewe si mhitimu tena wa Chuo Kikuu cha Exploits na kwa hivyo cheti chako cha digrii kimebatilishwa mara moja."kauli ilitolewa na Desmond Bikoko ambaye ndiye msimamizi wa shule hiyo.

Kulingana na watumizi wa mitandao walionesha kumkashifu msichana huyo wakisema kitendo chake hakikuwa chenye busara hata kama kazi iliwa nadra sana kupatikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live