Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshukiwa wa mauaji ni baba wa mtoto wa Mohbad

Mohbad Res Mshukiwa wa mauaji ni baba wa mtoto wa Mohbad

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari za uchunguzi na mpelelezi maarufu wa Nigeria Kemi Olunloyo amefichua Siri kwamba Sam Larry ndiye anadaiwa kuwa baba wa mtoto wa Mohbad.

Haya yanajiri baada ya Mpelelezi huyo kusema awali kuwa mke wa Mohbad alikuwa na mahusiano ya kingono na wavulana wa Marlian.

Olunloyo ametoa madai haya katika chapisho lake la hivi punde la Instagram leo, Septemba 25, akiongeza kuwa uchunguzi wake umewasilishwa kwa Jeshi la polisi nchini Nigeria.

Ameandika mpelelezi huyo; 1. Nia ya kifo cha Mohbad ilikuwa nini? 2. Je, Ulikuwa ni Mpango wa kumuondoa Mohbad na mali zake zote alizopata kwenye muziki ili zihamishiwe kwa mtoto na mke ambaye alimsaliti na kuwa na mtoto anaedaiwa kuwa ni wa Sam?

3. Sam angerithi mali zote za Mohbad akiwa kama baba wa mtoto, na kwanini nime watahadhari wanaijeria kuhusu kuchangia pesa kwa mama na mtoto. Ni Kwasababu Kiasi cha N30M kinatakiwa kishikiliwe na benki kwasababu mtoto hajapoteza baba.

4. Zikowapi simu za Mohbad baada ya kusafirishwa kwenda na kutoka hospitali? 5. Je, Mohbad alizikwa akiwa hai baada ya kuchomwa dawa ya midolazam zilizoleta mijadala kuwa zilimpelekea kupoteza fahamu na Kisha kuhangaika? Maana Shingo Yake kwenye jeneza ilionekana imevunjwa.

6. Kwanini Naira Marley alikaa kimya kuhusu vipimo vya DNA vilivyofanyika Dubai na alikuwa na makaratasi (Copy) Ya Vipimo 7. Kwanini Sam Larry alikuwa anagombana na Mohbad kuhusu Mtoto wake ambapo na Mohbad aligoma kumkabidhi mtoto huyo?

Kwa mujibu wa Rekodi zangu za Benki-UBA 8. Kwanini kuhani mkuu wa cubana alimpa baba yake Mohbad N4M (Tsh Mil 12) siku kadhaa kabla ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha Mohbad?

9. Kwa nini alidanganya kuwa Davido pekee ndie aliyempa N2M (Tsh 6.2m) ambayo alikuja sema baadae kuwa N1M (Tsh Mil 3.1/=) pekee ndio iliyowasilishwa kwake?

10. Kwa nini Samusi kijana mwenye Dread alisafiri Hadi Dubai muda huo huo baada ya Mohbad kuuawa? Yule Jamaa mwenye Dread anatajwa kuwa ni mpiga dili wa Dubai na pia alionekana kwenye gari lililokuwa na mwili wa Mohbad

Mpelelezi huyo akamalizia kwa kusema amewasilisha upelelezi wake kwa Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Lagos kuhusu Sam Larry mshtakiwa wa Mauaji ya Mohbad na rafiki wa karibu wa Naira Marley.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live