Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshukiwa kifo cha Mohbad akamatwa

Mauaji Mohbad Mshukiwa kifo cha Mohbad akamatwa

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Jimbo la Lagos kupitia Kamanda wake SP Benjamin Hundeyin wamethibitisha kumkamata Sam Larry ambaye ni rafiki wa karibu wa Naira Marley kwa sababu ya uchunguzi unaoendelea kubaini chanzo cha kifo cha Msanii Mohbad.

Hundeyin kupitia taarifa hiyo amesema; "Ndiyo, Balogun Eletu almaarufu kama Sam Larry sasa yuko chini ya ulinzi wetu. Kwa sasa anasaidia uchunguzi unaoendelea.”

Inadaiwa sababu ya kukamatwa kwa Sam Larry ni pamoja na kuwahi kushtakiwa na Mohbad kwa kumpiga na kumtisha kifo ambapo mara kadhaa pia alikuwa chanzo cha kumkosesha amani msanii huyo.

Aidha, sababu nyingine ya kukamatwa kwake ni kudaiwa pia kuwa baba halali wa mtoto wa Mohbad.

Sam Larry anaungana na muuguzi aliyemchoma sindano Mohbad huku watuhumiwa wengine wanaosubiriwa kukamatwa ni pamoja na Naira Marley aliyesema hivi karibuni ana mpango wa kurudi nchini humo kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha msanii huyo. Mke wa Mohbad pamoja na watu wa karibu waliokuwepo wakati wa Kifo cha Mohbad.

Mohbad, 27, alifariki tarehe 12 Septemba na kuzikwa siku iliyofuata huko Ikorodu, Jimbo la Lagos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live