Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi Miss Tanzania kuzawadiwa gari

Ec93ac3b0ca0a95921b90a63f4a47606 Mshindi Miss Tanzania kuzawadiwa gari

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHINDI wa shindano la Miss Tanzania 2020 atazawadiwa gari aina ya Subaru.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam, jana na waandaaji wa shindano hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basilla Mwanukuzi wakati akitangaza kambi rasmi ya warembo 20 watakaochuana katika fainali ya shindano hilo Desemba 5 mwaka huu kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Alisema mbali na gari, pia kutakuwa na zawadi ya kiwanja iliyotolewa na Dalali Msomi eneo la Kigamboni, masofa yaliyotolewa na Bai Furniture, fedha, viatu na nguo kutoka kwa wadau wengine waliowaunga mkono.

“Tumepanga kutoa zawadi ya gari kwa mshindi wa jumla, lakini pia tunawashukuru wadau wetu mbalimbali waliotuunga mkono wakiahidi kila mmoja kutoa zawadi, naamini shindano litakuwa zuri na la aina yake, tunahimiza Watanzania kuanza kununua tiketi kuanzia sasa,” alisema.

Basilla alisema kutakuwa na vipengele tofauti vitakavyoewaniwa ikiwamo kipya walichokianzisha cha kuulizwa maswali ya papo kwa papo, mrembo mwenye malengo, mrembo mwenye kipaji, mrembo mwenye mvuto, mrembo mwanamichezo na mrembo mwenye muonekano wa kuvutia.

Alisema wale watakaoshinda kwa kila kipengele watakuwa na nafasi ya kuingia kwenye 10 bora.

Mshindi wa jumla anatarajiwa kuwakilisha nchi katika shindano la urembo la dunia litakalofanyika Oktoba mwakani kwani mwaka huu halitokuwapo kutokana na janga la corona.

Kwa upande wake, mrembo anayeshikilia taji hilo, Sylvia Sebastian aliwatakia heri warembo wote 20 waliongia kambini wafanye vizuri.

Alisema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na tofauti kutokana na kipengele hicho kipya hivyo ana amini yatawajenga warembo kujiamini.

Chanzo: habarileo.co.tz