Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshikemshike tuzo za Afrimma leo

Mshikemshike tuzo za Afrimma leo

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii gani wa Tanzania kurejea na tuzo za Afrimma zinazofanyika leo Jumamosi Novemba 23, 2019 mjini Lagos, Nigeria.

Wasanii kutoka nchi 26 barani Afrika watachuana katika tuzo hizo huku Tanzania ikiwa na wasanii 11.

Wasanii hao ni Maua Sama aliyeingia katika tuzo hizo kwa wimbo wake wa Ikote, Nandy (Aibu); Rosa Ree (Dip in Wine It); Vanessa Mdee (Moyo) na Queen Darleen (Mbali).

Wasanii hao wa kike wanawania kipengele cha  msanii bora wa kike Afrika Mashariki wakichuana na  Sheebah na Irene Namatovu wa nchini Uganda.

Wasanii wa kiume wanaowania kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki ni Diamond (Inama); Harmonize (Never give Up);  Rayvany (Tetema); Mbosso (Hodari), Omy na Dimpoz (Ni wewe).

Katika kipengele hicho, wasanii hao wa kiume wa Tanzania watachuana na Roy Black na Shy wa nchini Madagascar na Khaligraph na Nyashinski wa Kenya.

Wengine waliochomoza katika tuzo hizo ni kundi la Navy Kenzo katika kipengele cha Best Reggae Ragga au  Dancehall kupitia wimbo wa Roll It, kipengele  ambacho pia yupo Rosa Ree. 

S2Kizzy, ambaye ni mtayarishaji wa muziki wa Tanzania anawania kipengele cha mtayarishaji bora  kupitia wimbo wa Tetema huku mwongozaji wa wimbo huo, Kenny naye anawania kipengele cha mwongozaji bora wa mwaka.

Kipengele cha maDJ bora kinawaniwa na Romy Jones.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz