Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msechu awajibu wanaosema hamtoshelezi mkewe

Afer Msechu Msechu na mkewe.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amefunguka kuhusu matusi ambayo amekuwa akitukanwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuonekano wake na familia yake kwa ujumla.

Akifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram, Msechu amesema kuwa watu hao anawasamehe na kumwachia Mungu, lakini kwa kumtukana wamekuwa wakimuongezea hasira ya kupambana ili aweze kufanikiwa zaidi na kuitunza familia yake.

"Kuna vijana wa kike kwa wa kiume hapa Instagram wa umri wangu kabisa na tena wengine wamenizidi kielimu na kiumri kabisa wanakesha kila siku kunitukana kwamba mimi bonge nina kitambi, sijui nafanyeje mapenzi na mke wangu, mara sijui sina mvuto, mara sijui kuvaa, mara sijui puto limefeli, mara sijui siwezi kupendwa na wanawake wengine.

"Wengine wakaenda mbali wakasema Mama Lolo atakuwa na mahusiano nje kwa sababu mimi simtoshelezi, wengine wakasema watoto sio wangu wale, wengine wakasema nitakufa kwa presha na kisukari hivi karibuni kwa kifupi nimeshatukanwa kila aina ya tusi chafu, tusi la nguoni, tusi la kila kabila nimeshatukanwa.

"Ninachoweza kusema kwa yeyote aliyewahi nitukana kipindi cha nyuma, ambaye atanitukana leo, ambaye atanitukana kesho, keshokutwa na kuendelea hadi milele ninachoweza kusema ni ahsante.

"Ahsante kwa sababu gani? Ni kwa sababu matusi yenu yanaendelea kunipa nguvu ya kuendelea kuipambania familia yangu watoto wangu na mke wangu waishi maisha matamu na mazuri kwa sababu hao pekee yao ndio wanaijua tahamni yangu na umhimu.

"Wako katika ujenzi wa familia yangu, Peter Msechu. Jumamosi saa 16:00 Helsinki Finland," amesema Msechu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live