Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msechu atozwa Sh1 milioni kwa kuimba wimbo bila ridhaa ya wahusika

52980 MSECHU+PIC

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, Peter Msechu ameilipa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Atomic Jazz Band ya Tanga Sh1 milioni kwa kukarabati na kuimba wimbo wao wa ‘Tanzania Yetu’ bila ruhusa yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe leo Alhamisi Aprili 18, 2019 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake 2019/2020.

Amesema hatua hiyo imetokana na Chama cha Hatimiliki Tanzania (Cosata) ambacho kiko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kutatua migogoro ya wasanii.

Ametaja migogoro mingine iliyotatuliwa na Cosata ni pamoja na Akim Igembe kumlipa Anna Joseph Sh 6 milioni kwa kuwahisha sokoni filamu yake iitwayo Naina bila ruhusa yake.

“Murchy Ben International imemlipa Jenista Raymond Mao Dola za Marekani 1,500 kwa kuingiza mtandaoni filamu yake ya Perfect White bila kibali chake,” amesema.

Dk Mwakyembe amesema kamati ya mikataba bado haijafikia maridhiano na kampuni saba kwa kazi za marehemu King Majuto.

Amezitaja kampuni hizo kuwa ni Freedom Film Production, Afsar Furniture, Sterling Surfactants Ltd, Al Riyamy Production na Al Abdis Entertainments.

Ametaja maridhiano mengine ni kati ya kazi za marehemu Steven Kanumba na kampuni ya Startimes na kazi za Wastara Juma na kampuni KZG Service Ltd.

Amezitaka kampuni hizo zifikie makubalianona kamati mapema iwezekanavyo bila kulazimika kuzipeleka mahakamani.

“Nawahimiza vilevile  wadau wote  wa sanaa kuhakikisha hawaingii mikataba yoyote bila ushauri wa kisheria. Nitumie fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wajumbe wa kamati hii kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya kwa kujitolea na kwa uadilifu mkubwa,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz