Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii wa Wagonga ulimbo,Dakika 90 afariki dunia

NYANDU BOY Msanii wa Wagonga ulimbo,Dakika 90 afariki dunia

Mon, 18 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akitoa taarifa kuhusu chanzo cha kifo chake, ratiba ya mazishi na msiba ulipo msemaji wa familia aitwaye Noster amesema

"Chanzo cha kifo chake ilikuwa ni ajali ya gari iliyotokea saa 12 jioni wakati anatoka beach, gari ilimshinda dereva ikaacha barabara na ikaenda kupiga miti, yeye alitaka kuruka ila miti ya pembeni ikapiga kichwani mwake, msiba upo nyumbani kwao Tegeta Dar Es Salaam na ratiba ya mazishi itakuja muda mfupi maana kuna ndugu zake walikuwa mbali na tunawasubiria" ameeleza Noster

Kupitia tamthilia ya Wagonga ulimbo marehemu alikuwa ni kamera man ambaye ameshiriki ku-shoot tamthilia hiyo mwanzo mwisho, na kwenye tamthilia ya Dakika 90 alikuwa ni mshiriki ambaye alitumia jina la Nyandu Boy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live