Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii wa Nandy Yammi alalamika shoo yake kubuma kisa mvua

Msanii Wa Nandy Yammi Alalamika Shoo Yake Kubuma Kisa Mvua Msanii wa Nandy Yammi alalamika shoo yake kubuma kisa mvua

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yammi, msanii wa lebo inayomilikiwa na Nandy amelalamika vikali baada ya mvua ya ajabu kuikatisha shoo yake ya kwanza nje ya Tanzania.

Shoo hiyo kwa jina Zii Jam ilikuwa imeandaliwa na Ziiki Media katika jiji la Mombasa, Kenya na Yammi alikuwa miongoni mwa wasanii walioalikwa kutumbuiza wakiwemo Rayvanny, Otile Brown miongoni mwa wengine wikendi iliyopita.

Sasa Yammi kwa ishara zote aliashiria kwamba mvua hiyo haikuwa ya kawaida akionekana kuihusisha na mikosi ya ushirikina.

Alipakia video kwenye Instagram yake ikionyesha mvua ikinyesha na kusema kwamba mvua zilizanza tu pindi alipopanda jukwaani na kuacha kunyesha alipomaliza kutumbuiza.

“Imefika zamu yangu ya kuperfom sijui ata mvua ilitoka wapi, nimeperfom huku nanyeshewa mvua ,nilipomaliza tu mvua yote ikakata....Mimi peke angu Ndo msanii nilonyeshewa na mvua,” alilalamika.

Hata hivyo, Yammi aliwashukuru mashabiki wake wa Mombasa kwa mapokezi mazuri akiahidi kurudi tena katika mwendelezo wa shoo zake nje ya nchi

“Asanteni Mombasa pamoja na mvua yote lakini mlisogea mkakubali kunyeshewa kwaajili yangu nawapenda sana,” Yammi alishukuru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live