Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii mrembo aliyefungwa jela kwa kuonesha nguo ya ndani

194 Pop Singer Arrested For Dancing In Undies And Eating Banana Suggestively TZW

Fri, 15 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Mahakama nchini Misri imemuhukumu kifungo cha miaka miwili  jela mwimbaji Shaimaa Ahmed ambaye kimuziki anafahamika kama Shyma baada ya kuonekana kwenye video akiwa na vazi la ndani huku akila ndizi.

Alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo. Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.

Director wa video hiyo pia nae alihukumiwa kifungo cha miaka miwili licha ya yeye kutowepo mahakamani.

Shyma alikuwa ameomba msamaha kabla kukutwa na hatia.

“Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwaa kwa njia hii kali kutoka kwa kila mtu.” – Shaimaa Ahmed

Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngino kwenye video ya muziki.

Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.

JPM AONYA WASICHANA WANAOJIACHIA KWENYE VIDEO,SIX-PACK ZA WANAUME JE?, BONYEZA PLAYA HAPA CHINI KUMTAZAMA.

Chanzo: millardayo.com