Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri -Tammy The Baddest

5498 Tammy Bongo5 Jpg TZW

Thu, 29 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Female Rapper Tammy The Baddest amesema muonekana wa msanii mbele ya mashabiki wake una nafasi katika kuuza muziki wake anaofanya.



Tammy amesema kuwa msanii si kuandika nyimbo tu na kuingia studio kurekodi bali hata muonekano wake ni kitu cha kuzingatia.

“Msanii kama msanii hasa mtoto wa kike unatakiwa uwe full package, sio unaonekana tu umefanya muziki basi, no!, you have to sale, ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri hata kama una shida mtu aone mmmh!, kumpa Tammy show kiasi fulani hapana,” Tammy ameiambia Bongo5.

Ameongeza kuwa muuoneka wake ndio kila kitu kwake japokuwa muda mwingine inakuwa tabu kwake kwa kuwa baadhi ya mashabiki wake hufikiri ana fedha nyingi kitu ambacho si kweli.

Chanzo: bongo5.com