Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Msanii haondoki WCB bure, nimewekeza hela yangu’ - Diamond

Diamond D Voice Diamond na D Voice.

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa bongo fleva Diamond Planumz ameweka wazi na kutilia mkazo suala la madai kwa msanii yeyote aliyeko anayesimamiwa na lebo ya WCB pindi atakapoamua kuondoka, kama ilivyotokea kwa wasanii wengine takriban watatu waliositisha kuendelea kufanya kazi na mwimbaji huyo.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo cha Wasafi Tv Diamond ambaye jina lake halisi ni Nassibu Abdul Juma amesema kuwa mwanzo uelewa wa sehemu kubwa ya wadau na mashabiki kuhusu biashara ya muziki ulikuwa chini na ndio sababu alipitia kipindi cha kulalamikiwa kuwa anawanyonya wasanii waamuapo kujitoa katika lebo hiyo.

“Pengine mwanzo ilikuwa ni upya wa Industry watu kutoelewa, nakumbuka wakati mmoja msanii mmoja wakati anatoka, akawaambia kwamba anatakiwa kulipa kiasi cha pesa, sasa wale walikuwa hawajua vizuri nikakutana nao nikawaambia kuna miziki miwili, kuna muziki na muziki ndani ya Wasafi, Muziki ndani ya wasafi watu wanapata riziki”

“Nikawaambia huyu msanii unayemzungumza sasa hivi YouTube yake kwa mwezi inatengeneza sio chini ya milioni arobaini na nane, wewe unaniambiaje kila mwezi hiyo Miulioni arobaini na nane niiache, msanii hawezi akaondoka hivi hivi, nimewekeza hela yangu ya kutosha mpaka anafanikiwa na kuingiza Mamilioni Ya Fedha,” amesema Platnumz.

Mwimbaji huyo mwisho mwa juma lililopita alifanya hafla ya kumtambulisha rasmi msanii wake mpya D voice, hafla iliyoudhuriwa na wasanii na watu mashuhuri kutoka katika tasnia mbali mbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live