Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii asimulia alivyotobolewa jicho kwa wizi

Msanii Asimulia Alivyotobolewa Jicho Kwa Wizi.png Msanii asimulia alivyotobolewa jicho kwa wizi

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii Daddy Owen kwa mara ya kwanza amefunguka mazingira yaliyopelekea yeye kupoteza jicho moja.

Owen katika mazungumzo na Obinna, alisimulia kwamba kitambo kabla ya kupata wokovu alikuwa mwizi kibaka wa kuibia watu mikoba na simu kwenye hadhira.

Wakati mmoja baada yake na wenzake kwenda kwenye mkutano mmoja na kujaribu njama yao, ilikula kwake na hapo ndipo alipovamiwa na watu waliompa kichapo hadi kupelekea kupoteza jicho moja.

“Katika moja ya wizi, ndio nilipoteza jicho langu moja. Ilikuwa ni tamasha tulikuwa tumeenda, unaua zile siku ilifika mahali tulikuwa tunalenga katika matamasha makubwa. Kwa sababu unajua watu wakienda matamasha haya makubwa ni lazima watakuwa walevi na hiyo ilikuwa rahisi kuwaibia kwa sababu nyakati hizo watu walikuwa wanatembea na pesa taslimu…” Daddy Owen alisema.

“…Kwa hiyo ukipata vibeti kama 5 uko sawa, ukiambia mtu kuwa weka mikono juu hapo uko na uhakika utampata na pesa. Huo ndio ulikuwa mpango. Lakini mpango huo ulitibuka nikashikwa nikapigwa na halaiki hadi kupoteza jicho,” Owen aliongeza.

Msanii huyo alisema kwamba aliponea kuteketezwa kwa sababu tukio lilitokea nyakati za usiku.

“Walinipiga wakaniacha hapo kwa sababu walifika mahali wakajua kwamba huyu tumemmaliza. Baadae mlinzi mmoja alikuwa na roho ya utu alikuja akaniweka kwenye nyuma ya kibanda nikakaa saaa kadhaa ndio nikapanda gari nikaenda nyumbani. Sikuwa nimejua kwamba nimetobolewa jicho kwa sababu nilikuwa nimefura mwili wote. Baada ya siku mbili ndio nilikuja kugundua jicho haliko,” alisema.

Owen alisema licha ya kipindi hicho kuishi na baba yake, hakuwahi jua kwamba mwanawe amepoteza jicho kwani muda mchache baadae waliondoka katika nyumba ya wazazi wao na kwenda kupanga nyumba yao kando yeye na ndugu yake mkubwa Rufftone.

Chanzo: Radio Jambo