Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii aliyesambaza picha za uchi aomba radhi baada kufungiwa

1244 Screen Shot 2018 01 07 At 20.12.29.png TZW

Mon, 8 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii filamu na video vixen, Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha mitandaoni za nusu uchi.

Pretty Kind

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungiwa na serikali kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind amesema kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo sasa hataweza kurudi tena kufanya mambo hayo.

“Naomba niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua nimefanya kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa mashabiki zangu kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty Kind mwingine mpya na kufanya yale yanayotakiwa katika jamii” alisema

Pretty Kind amefungiwa kujihusisha na sanaa kwa takribani miezi sita baada ya kuposti picha katika mtandao wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania na kwenda kinyume na maagizo ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliyatoa hivi karibuni kuwataka wasanii wa kike kuvaa kwa staha.

Chanzo: bongo5.com