Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii afariki kwa kujinyonga

Abel Zakayo Abel Zakayo.

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Maigizo Mkoa wa Iringa, Abel Zakayo Mlasu (26) amejinyonga Oktoba 21 na kuzikwa Oktoba 22, huku ugumu wa maisha ikitajwa sababu ya kujinyonga kwake.

Abel amejinyonga kwa kutumia mtandio katika paa la nyumba aliyokuwa akiishi yeye na mama yake mzazi, uongozi wa mtaa umethibitisha kifo hicho.

Fredy Saimon aliyekuwa mtu wa karibu na marehemu alisema, Abel alianza kubadilika na kuanza kunywa pombe na kuonekana kama mtu mwenye msongo wa mawazo.

Fred ambaye ni kiongozi wa Wasanii wa Filamu mkoani humo amesema Abel alikuwa akiishi na mama yake na kutokana na changamoto za maisha alibadilika.

Mama mzazi wa Abel, Elina Mvela amesema Oktoba 18, mtoto wake alitoka kwenye mizunguko na kurudi nyumbani, lakini akiwa amebadilika na kuwa mtu aliyechanganyikiwa ndipo alichukua hatua ya kumfunga kamba na kumfungia chumbani na baada ya muda alimuona ametulia na kumpa chakula.

Siku ya tukio mama huyo anasema aliamka kwenda kwenye mizunguko lakini aliporudi nyumbani alikuta Abel amejifungia mlango na ndipo walipofanya juhudi za kuvunja mlango na kukuta amejinyonga kwa kujitundika katika paa la nyumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live