Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii aeleza alivyoacha kubadili dini baada ya kupata pesa

Msanii Aeleza Alivyoacha Kubadili Dini Baada Ya Kupata Pesa Msanii aeleza alivyoacha kubadili dini baada ya kupata pesa

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Omah Lay ameweka wazi kuwa amewahi kufikiria kubadilisha dini kutoka katika Ukristo na kuwa Muislam.

Msanii huyo ameeleza hayo kufuatia mahojiano yake na mwandishi wa habari Wunmi Bello, Omah alifichua suala hilo la kufikiria kubadilisha dini licha ya kuzaliwa na kukulia katika familia ya kikristo.

“Nilitumia muda mwingi kanisani, na wakati fulani nilifikiria kubadili dini lakini sasa niko katika hatua ambayo ni mimi tu na Mungu na siyo dini”

Katika mahojiano hayo Omah ameeleza kuwa mara tu baada ya kupata pesa alibadilika na kuanza kumuamini Mungu hivyo basi kwa sasa hajali kuhusu dini.

Stanley Omah Didia, maarufu kama Omah Lay, amejulikana zaidi kupitia nyimbo zake kama ‘Godly’ ‘Damn’ , ‘Reason’ na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live